Blue Economy
Unajua nini kuhusu uchumi wa buluu?
Blue Economy ( Uchumi wa Buluu) ni shughuli za kiuchumi zinazohusu matumizi bora ya rasilimali za bahari kwa ajili ya kuimarisha au kukuza uchumi.
Zanzibar, kwa mfano sekta ya uvuvi huchangia 2.6% ya pato ghafi la Zanzibar, hutoa ajira za moja kwa moja kwa watu 200,000 wakati zaidi ya watu laki 4 hutegemea sekta hii.
Kuna nafasi kubwa na nzuri ya kuifanya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuwa na uchumi mzuri zaidi kwa kuifanyia maarifa zaidi Blue Economy.
Baadhi ya hoja kuu zilizoibuliwa kwenye Sustainable Blue Economy Conference Nairobi Mwezi November 2018.
A. Dolari za Kimarekani Billion 23 hupotea kwenye uchumi wa dunia kila mwaka kwa uvuvi haramu.
B. Zaidi ya aina million 2.2 za wanyama, mimea na wanyama wengine huishi baharini
C. 2% ya wanawake duniani hujihusisha na shughuli za bahari
D. Watu Billion 3.1 huishi ndani ya km 100 kutoka baharini.
E. 90% ya biashara yote duniani hupitia baharini na inaongezeka maradufu kufikia 2030.
Bahari na uchumi endelevu wa bahari ni kiini cha uchumi wa kileo.
Thanks for your knowledge
ReplyDelete