Maajabu ya bahari
MAAJABU YA BAHARI KATIKA DUNIA Uchumi wa Bluu; Maajabu ya bahari. 0 TAFITI zimebaini kuwa asilimia 71 ya uso wa dunia ni maji na asilimia 97 ya maji hayo ni bahari. Ikimaanisha, eneo la nchi kavu ni asilimia 29 tu ya uso wa dunia. Hiyo inamaanisha nini? Kama bahari itatumika ipasavyo, basi kuna uwezekano wa uchumi wa dunia kutotegemea kwa kiasi kikubwa rasilimali zilizoko nchi kavu. Kama ambavyo imekuwa ikionekana, matumizi ya bahari yamekuwa na tija na mchango mkubwa kwenye uchumi wa mataifa mbalimbali duniani kote. Mathalan, unaweza kuona namna shughuli za uvuvi, uchimbaji mafuta, utalii na uchukuzi na usafirishaji zinavyoiingizia fedha za kigeni Tanzania, achana na kuwa chazo kizuri cha ajira. Kwa kudokeza tu, zipo tafiti za kuaminika zinazoeleza kuwa shughuli zihusianzo na bahari huchangia takribani Dola za Marekani Trilioni 2.5 katika uchumi wa dunia. Katika kuhusianisha bahari na maendeleo ya kiuchumi, ndipo inapoibuka dhana ya Uchumi wa Bluu. Ni kitu gani hicho? Uchumi wa ...